Mugabe aita wabunge kuwapa hotuba sahihi

Mugabe aita wabunge kuwapa hotuba sahihi

1.2kViews
 
ZIMBABWE – Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amewaita wabunge wa nchi hiyo kwa kikao maalum siku moja baadaye yake kuwasomea hotuba isiyofaa, kimakosa.

 

Anatarajiwa kusoma hotuba iliyo sahihi wakati wa kikao hicho leo.

Haijaeleweka ni vipi Bw Mugabe aliishia kusoma hotuba isiyofaa wakati wa kufunguliwa kwa bunge, lakini msemaji wake alikuwa ameambia gazeti la serikali la Herald kwamba kosa hilo lilitokana na suitafahamu katika afisi ya kiongozi huyo.

Kiongozi huyo aliaibika sana baada yake kurudia hotuba hiyo aliyokuwa ameisoma awali Agosti 25 wakati wa kikao cha kufafanua kuhusu hali ya taifa.

Kituo cha utangazaji wa serikali nchini humo kimewataka wabunge kufika kuhudhuria kile kilichotajwa kuwa kikao kisicho cha kawaida cha bunge.

  love 0 Love
  wink 0 Wink
  lol 0 LoL
  wow 0 Wow
  cry 0 Cry
  angry 0 Angry